KATIBU Tawala mkoa wa Tanga Rashidi Mchatta amewasisitizia wakulima wa zao la korosho kuuza korosho baada ya kuziongeza thamani ili kuona faida tofauti na kuuza korosho ghafi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).
Akizungumza wakati alipotembelea banda la bodi ya Korosho katika maonyesho ya Nanenane kanda ya mashariki mjini Morogoro ambalo ni moja ya mazao ya kimkakati Mchata amesema uuzaji wa korosho zilizoongezwa thamani utawanufaisha zaidi wakulima kupitia mauzo yatokanayo na korosho kwamba uzalishaji kwa mwaka huu unatarajia kuongezeka .
Akieleza hali ya uzalishaji wa zao hilo kwa Kanda ya Mashariki Meneja wa tawi la bodi ya korosho mkoa wa Morogoro Japhari Matata amesema mkulima anayeweza kuuza kilo 500 za korosho ghafi nakupata shilingi Milioni 1.1 na kwamba akiuza baada ya kuziongezea thamani anapata shilingi Milioni 3.5.
Amewahimiza wakulima kuona umuhimu wa kubangua korosho na kuziuza na kuona thamani ya zao hilo.
Zaidi ya tani 610 za korosho zimezalishwa katika msimu wa kilimo mwaka jana na kwamba kwa mwaka huu uzalishaji unatarajia kuongezeka kutokana na wakulima kujipanga kuongeza uzalishaji.