MAHAKAMA Kuu Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajia kutoa uamuzi wa maombi ya Said Issa Mohammed na mwenzake ya kutaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzuiwa kufanya shughuli za siasa tarehe 22 Oktoba 2026.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Waombaji hao wamerejea tena kortini baada ombi kama hilo kutupwa ambapo walikuwa
Wakilalamikia mgawanyo wa rasimali za Chadema usio sawa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara huku wakidai kuwa Zanzibar inapunjwa.
Tarehe 28 Mei 2026, Mahakama kuu mbele ya Jaji David Ngunyale ilitupilia mbali shauri hili na kueleza kuwa halikufunguliwa kwa misingi ya kisheria.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa saa 2 asubuhi mbele ya jaji Awamu Mbagwa.
Mwisho.