Rais Samia Suluhu Hassan
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa Viongozi saba katika Utumishi wa Umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo 22 Julai 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka imesema Dk. Latifa Mohammed Khamis ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano.
Prisca Burton Lwangili ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Aidha, Abdallah Hassan Mitawi amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, wakati Balozi Baraka Haran Luvanda amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.
Vilevile, Dk. Franklin Jasson Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, huku Dk. Maduhu Isaac Kazi akihamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Mazingira.
Katika uteuzi huo pia, Ephraim Balozi Mafuru ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), akitokea Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ambako alikuwa Mkurugenzi Mkuu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.