Tundu Lissu akiwa mahakamani
MKUU wa Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam, amenusirika kuhumiwa kifungo gerezani na Mahakama Kuu, Maslaja Ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkuu huyo wa Gereza aliponzwa na msimamo wake wa kung’ang’ania kutoruhusu mawakili na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kumtembelea mshitakiwa gerezani.
Kimbembe hicho, kilimkuta mkuu wa gereza wakati akihojiwa maswali ya dodoso na Lissu, katika shauri la kikatiba na 7300/2026, lililofunguliwa Mahakama Kuu na mawakili wake watatu, wakiongozwa na Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo.
Akihojiwa na Lissu mbele ya jopo la majaji watatu, Andrew Tamanjiro, Mkuu wa Gereza Kuu la Ukonga, alisema kuwa hawezi kumruhusu mtu yoyote kumtembelea mshitakiwa huyo gerezani.
Kesi hiyo, iliyoibuka baada ya Lissu kushitakiwa kwa uhaini, iko chini ya majaji Amir Mruma, Dk. Angelo Rumisha na Evarist Longopa.
Mahojiano kati ya Lissu na Mkuu wa Gereza (Bw. Jela), Andrew Shabani Tamanjiro, yalikuwa kama ifuatavyo:
Lissu: Karibu ipi ambayo hawasikii?
Bwana Jela: Unaweza kuwa karibu na usisikie.
Lissu: Kuna mawakili 37 ambao umeleta nyaraka zao hapa pamoja na mawakili wangu.
Sasa kwenye andishi lako, umekuwa ukisema simamia kwa karibu, simamia mazungumzo yao. Ni kweli kwa mawakili wote?
Bwana Jela: Sio kweli, lakini ni kweli naomba niseme ni kweli nimesema komenti hizo kwa wote.
Lissu: Katika mawakili wote hao, kuna mahali hata pamoja ulipoandika simamieni, lakini msisikilize mazungumzo yao?
Bwana Jela: Hakuna.
Lissu: Je katika mawakili wote 37 umeandika wakiingia ofisini tokeni nje wazungumze? Kuna sehemu umeandika?
Bwana Jela: Hakuna nilipoandika.
Lissu: Kuna mahali kokote umeelekeza kuwa angalieni lakini msisikilize?
Bwana Jela: Hakuna mahali hapo.
Lissu: Waeleze majaji kama ni kweli au sio kweli kati ya tarehe 18 Aprili 2025 nilikuwa nazungumza kwenye kioo na mawakili wangu?
Bwana Jela: Kilikuwepo hicho kipindi.
Lissu: Tulikuwa tunawasiliana kupitia simu zilizopo pale?
Bwana Jela: Kweli.
Lissu: Je upande anaokuwepo mgeni ndio uko karibu na mapokezi na kuna kachumba ambacho ni control room ya hizo simu zote na kwenye hilo eneo, anakuwepo Afisa Magereza anayeuwasha na kuuzima. Ili watu wazungumze yeye ndio anaamua hapo.
Bwana Jela: Ni kweli.
Lissu: Huyo wakili anapozungumza kuna askari wanakuwepo kumsikiliza?
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Je, huu upande wangu nakuwa pia na askari wananisikiliza niliotoka nao lockup na wengine wananisikiliza?
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Kwenye hicho chumba kuna CCTV Camera inayorekodi kinachoendelea humo?
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: CCTV camera hiyo iko controlled ofisini kwako? Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Je, ni kweli kwamba baada ya matukio ya 29 Oktoba, uliniita ofisini kwako?
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Ulivyoniita ukaniambia kuanzia sasa ni marufuku viongozi wa Chadema na wanachama wa Chadema kuja kukutembelea.
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Na pia ulisema ni ndugu zako wa karibu tu ndio watakutembelea?
Bwana Jela: Sio kweli.
Lissu: Na ukasema mazungumzo yako na mawakili yatakuwa kwa mambo ya kisheria tu?
Bwana Jela: sio kweli.
Lissu: Wakili Gaston Garubindi alikuwa anakuja kunitembelea Gerezani kabla ya tarehe 14 Novemba 2025.
Bwana Jela: Kweli.
Lissu: Kuanzia hiyo tarehe hajawahi kuruhusiwa? Bwana Jela: Simpangii.
Lissu: Kuanzia niingie gerezani Wakili Dickson Matata na Deogratias Mahinyila, hujawahi kuwaruhusu waingie gerezani. Huyu Matata ni Mwenyekiti Kanda ya Magharibi na Mahinyila ni Mwenyekiti wa Vijana Taifa (Bavicha), hawajawahi kuruhusiwa?
Bwana Jela: Siwalazimishi waje au wasije.
Lissu: Kumbe ndio hivyo. Haya Mahinyila na Matata kesho njooni Ukonga.
Bwana Jela: Kesi iko mahakamani sitawaruhusu.
Lissu: John Heche, Amani Gorugwa, Katibu Mkuu Mnyika wakiwa kama mashahidi wangu kwenye kesi ya uhaini wamezuiwa kuingia?
Bwana Jela: Hawawezi kuingia.
Jaji Mruma: Hilo la kwamba huwezi kuruhusu umelitoa wapi? Kuna amri yoyote ya Mahakama?
Bwana Jela: Siwezi kuwaruhusu.
Jaji Mruma: Tumefikia huko. Unaiambia Mahakama kuwa huwezi kuruhusu na hauna amri yoyote ya Mahakama? Uko serious kweli au hujaelewa ili tufanye maamuzi na sisi sasa?
Bwana Jela: Waheshimiwa majaji naomba radhi. Jaji anamkata jicho.
Lissu: Soma hati yangu kinzani kuhusu Nashon Nkungu. Anasimama Wakili wa serikali tunaomba mapumziko. Majaji wanashauriana. Wakili John Seka anasema ni sawa tu. Naye Lissu anasema, hakuna shida.
Jaji: Basi tukutane mara baada ya saa moja.