KLABU ya Simba imetangaza kuwa tamasha la Simba Day 2026 litafanyika 8 Agosti 2026 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku likiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema hayo leo Jumatano 22 Julai 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akisema awali walikuwa na matarajio ya kufanyia tamasha hilo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na ukubwa wa tukio hilo, lakini uwanja huo upo kwenye matengenezo.
“Simba Day 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru,Kutokana na ukubwa wa tamasha hili duniani tunatamani kufanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, lakini kwa sasa upo kwenye matengenezo hivyo uwanja ambao utatumika ni Uwanja wa Uhuru,” amesema Ahmed.
Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee kwa kuwa litakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 90 ya Simba Sports Club, huku mashabiki wakitarajiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuadhimisha historia ya klabu hiyo.