MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia Tundu Lissu ameanza rasmi utetezi wake kwa kutoa ushahidi wake kwenye shauri la Uhaini linalomkabili kwenye Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu amenza kutoa ushahidi wake akiwa shahidi wa kwanza, mara baada ya Mahakama hiyo, kumkuta na kesi ya kujibu kwa mujibu kwa kifungu cha 312 cha kanuni ya adhabu kuna kesi iliyojengwa.
Kujitetea huko kwa Lissu kumekuja mara baada ya upande wa Jamhuri kuweka pingamizi kwa shahidi wa kwanza hadi wa saba ambao Lissu aliwataja Mahakamani hapo.
Mashahidi hao ambao upande wa Jamhuri uliwawekea mapingamizi mahakamani hapo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Dk. Philip Mpango makamu wa Rais mstaafu, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu mstaafu.
Wengine ni Inspekta Jenerali wa Polisi Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jenerali John Nkunda ambaye ni Mkuu wa Majeshi. Ni mjumbe wa Sekretarieti wa baraza la usalama wa Taifa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Mahakama hiyo imesema kuwa pingamizi hilo watalitolea uamuzi, hivyo Lissu anaweza kuendelea na shahidi wa nane na kuendelea kwa kuwa hawana mapingamizi yoyote.
Katika ushahidi wake Lissu alidai kuwa kushtakiwa kwake kumefanya nchi za jumuiya za ulaya, kusimamisha misaada kwa Tanzania.
“Marekani imesimamisha misaada takribani dola milion 700 kwa mujibu wa taarifa zangu kwa sababu ya mashtaka haya. Kwa sasa bunge la Marekani, linajadili mswada wa kuwawekea vikwazo serikali ya Tanzania na viongozi wake kwa sababu ya mashtaka haya,” alidai Lissu
Aliendelea kusema kuwa Dunia haiwezi kumpigania mtu kama ni wa hovyo au mharifu, bali Dunia inapigana kwa sababu yeye ni mtu wa heshima.
Shauri hilo limeahirishwa mpaka Jumatatu 24 Agosti 2026, saa tatu asubuhi ambapo Lissu ataendelea na ushahidi wake.