KUFUATIA kuwepo kwa taarifa za kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Emmanuel Nchimbi taratibu za kikatiba zinaweka wazi hatua zinazopaswa kufuatwa kujaza nafasi hiyo mara tu inapokuwa wazi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa Ibara ya 50(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,pale Makamu wa Rais anapojiuzulu,nafasi hiyo inakuwa wazi rasmi.
Mchakato wa kumpata mbadala wake unaongozwa na Ibara ya 50(4),inayomtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo ndani ya siku 14 tangu siku ambayo nafasi hiyo ilikuwa wazi.
Baada ya uteuzi huo kufanywa na Rais,hatua inayofuata ni kuteuliwa huko kuwasilishwa Bungeni ili kuthibitishwa ba kura za wengi za Wabunge mara tu baada ya Bunge kutoa ridhaa na uthibitishi huo,Makamu wa Rais mpya ataapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 48(2) ya katiba kabla ys kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake kiofisi.
Taratibu hizi za kisheria zinahakikisha kuwa hakuna pengo la kikatiba linalotokea katika safu ya uongozi mkuu wa nchi na kwamba mchakato mzima unazingatia misingi ya demokrasia na utawala wa sheria.