RAIS wa Samia Suluhu Hassan, ameridhia kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi aliyendika barua ya kufanya hivyo leo, tarehe 25 Agosti 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Katika barua yake iliyosamba kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Nchimbi alieleza kuwa amemuandikia barua Rais Samia akiomba kustaafu siasa na utumishi wa umma mnamo 4 Septemba 2026.
Katika barua yake hiyo Dk.Nchimbi alieleza kuwa ameridhisha kuwa Rais Samia anahitaji mabadiliko
Mwanzo mwa Januari, mwaka jana Rais Samia na Dk. Nchimbi walipitishwa na vikao vya CCM kuwania nafasi zao katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Taarifa iliyotolewa jioni ya leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka ilieleza kuwa Rais Samia ameridhia ombi la Dk. Nchimbi.
Taarifa hiyo ileleza kuwa mchakato wa Kikatiba utaanza kumpata Makamu mpya wa Rais.
Mwisho.