MAHAKAMA Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam imesema kuwa Tundu Lissu ambaye anashtakiwa kwa kosa la uhaini ana kesi ya kujibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 21 Agosti 2026, ambapo Mahakama hiyo imesema kuwa kwa mujibu kwa kifungu cha 312 cha kanuni ya adhabu kuna kesi iliyojengwa na hivyo kuna kesi ya kujibu.
Mara baada ya kusomwa kwa uamuzi huo Mahakama hiyo ilisema kuwa Mshtakiwa (Lissu) anatakiwa kuleta mashahidi wake wakati wa kujitetea kwa kuwa ni haki yake.
Akizungumza mbele ya Mahakama hiyo kuhusu utetezi wake Lissu alieleza kuwa, atajitetea mwenyewe kwa kuwa shahidi namba moja, kisha akaorodhesha idadi ya mashaidi wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Dk. Philip Mpango makamu wa Rais mstaafu na Kassim Majaliwa Waziri Mkuu mstaafu.
wengine Inspekta Jenerali wa Pilisi Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jenerali John Nkunda ambaye ni Mkuu wa Majeshi. Ni mjumbe wa Sekretarieti wa baraza la usalama wa Taifa, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), John John Mnyika (katibu Mkuu wa Chadema).
Amani Sam Golugwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Wegesa Heche Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Brenda Rupia