MAHARAMIA wa Kisomali wameiteka nyala meli moja ya kusafirisha mafuta yenye bendera ya Tanzania imetekwa nyara katika pwani ya Yemen. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo wanaofahamu tukio hilo, meli hiyo imetekwa nyara leo asubuhi.
Maafisa hao wamesema meli hiyo ya kibiashara imehamishiwa katika maji ya eneo la Bari, kaskazini mashariki mwa Somalia.
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza kwa sharti la kutotajwa majina, meli hiyo, inayojulikana kama MT ASANA, ilitekwa nyara Ijumaa baada ya kuondoka Mukalla nchini Yemen. Kwa sasa inashikiliwa karibu na pwani ya Caluula katika jimbo la Bari, lililo ndani ya eneo linalojitawala la Puntland.
Vyanzo hivyo pia vimesema meli hiyo ilitekwa na maharamia saba wenye silaha kutoka Somalia.
Haikufahamika mara moja ni wafanyakazi wangapi walikuwa ndani ya meli hiyo wakati wa tukio, wala iwapo kuna yeyote aliyejeruhiwa. Pia, hakukuwa na taarifa za haraka kuhusu uraia wa wafanyakazi waliokuwamo ndani ya meli hiyo.