Tundu Lissu akiwa mahakamani
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu leo 20 Julai 2026 amefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma kwa ajili ya shauri la Kikatiba kuhusu haki za Mawakili ikiwemo haki ya faragha pindi wanapomtembelea gerezani.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Shauri hilo limefunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo wakieleza kuwa mamlaka ya Magereza ya Ukonga jijini Dar es Salaam imekuwa ikikataa kuwapa faragha ya kuzungumza na mteja wao (Lissu).
Kikao cha Shauri hilo la Kikatiba kinaketi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya jopo la Majaji watatu (3) ambao ni Amir Mruma, Dk. Angelo Rumisha na Dk. Evaristo Longopa.
Tundu Lissu ameshikiliwa gerezani tangu 10 April 2025 kwa mashtaka ya uhaini na kufikishwa mahakamani mara kadhaa ambapo mbele ya majaji kwa nyakati tofauti amekuwa akieleza kunyimwa faragha ya yeye na Mawakili wake wanapomtembelea gerezani.
Ikumbukwe kuwa katika kesi ya uhaini, Lissu ambaye ni Mwanasheria na Wakili kitaaluma anajitetetea mwenyewe lakini ana jopo la Mawakili ‘washauri’ wa kisheria wanaomsaidia pia katika kufanya tafiti za baadhi ya taarifa katika wakati ambao yupo gerezani.