JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kuna gari la polisi lililochomwa moto na wananchi katika eneo la Mwenge, likifafanua kuwa habari hiyo ni ya uzushi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambaa kwenye mitaandao ya kijamii yenye maudhui ya ‘WANANCHI WACHOMA MOTO GARI YA POLISI MWENGE DAR ES SALAAM’. Taarifa hiyo si ya kweli na ina lengo la kuupotosha umma na kuleta taharuki kwa jamii.
Kutokana na kusambaa kwa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limesema hatua za kisheria na kisayansi zinaendelea kushughulika na watu au makundi yenye aina hizo za taarifa ili wahusika wakamatwe na kufikishwa kwenye mamlaka zingine za kisheria.