JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeonya watu au makundi yanayohamasisha vurugu nchini, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kudhibiti ghasia na uvunjifu wa amani kwa kushirikiana na mamlaka za kiraia.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo Jumamosi 4 Julai 2026 na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Sylvester Mangure, JWTZ imefichua kuwepo kwa kampeni za uhamasishaji na upotoshaji zinazofanywa na watu wasioitakia mema nchi, ambao wamekuwa wakilichafua jeshi hilo kwa kusambaza uvumi kwamba litahusika kuwalinda watu wanaopanga kufanya vurugu na ghasia.
Jeshi limeonya kuwa vitendo hivyo vya uchochezi vinalenga kuvuruga shughuli za kila siku za jamii, kusababisha madhara ya kibinadamu, uharibifu wa mali, na hatimaye kuporomosha uchumi wa taifa.
Jeshi hilo limewatoa hofu wananchi kwa kuwahakikishia kuwa mipaka ya nchi na usalama kwa ujumla ni shwari.