AFRIKA imeendelea kuthibitisha ubora wa kabumbu baada ya Morocco kuitoa Uholanzi nje ya mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia kwa mikwaju ya penalti 3-2 katika hatua ya mtoano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwenye pambano lililofanyika Uwanja wa Monterrey, mjini Guadalupe, Mexico, alfajiri hii, Morocco ilifanikiwa kurudisha goli dakika ya majeruhi baada ya kutanguliwa kwa goli lililofungwa na C. Gakpo dakika ya 72.
Kwenye upigaji wa penalti, Issa Diop alifunga penalti yake pamoja na Ismail Saibari, C. Talbi na C. Rahimi kwa upande wa Morocco huku mshambuliaji machachari Ashraf Hakimi na El Aynaouni wakipoteza.
Uholanzi taifa kubwa kisoka ambalo mpaka sasa halojawahi kubeba kombe hilo, licha ya kufika fainali mara tatu, ililoshindwa mpaka sasa kutwaa kombe hilo, ilifunga penalti zake kupitia kwa Weghorst na T. Koolmei na waliopoteza ni C. Summer, Q. Timber na J. Kluivert.
Pambano hilo lilitazamwa na watu 51,243. Mechi ya kwanza ya mtoano ilizikutanisha Brazil na Japan ambako Japan walitolewa nje baada ya kufungwa 2-1. Mbali na Morocco timu za barani Afrika zilizovuka ngwe ya makundi ni Senegal, Cape Verde, Misri, Ivory Coast, DR Kongo na Afrika Kusini ambayo imetangulia kutolewa na Canada kwa kufungwa 1-0 kwenye mechi ya mtoano.