Said Issa Mohamed
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa wito kwa wanachama na wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kesho 23 Juni 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi, kufuatilia mwenendo wa shauri la kesi inayohusu mali za chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya chama, shauri hilo lilifunguliwa na Said Issa Mohamed pamoja na mwenzake, likihusisha mgogoro wa mali za chama ambao unaendelea kusikilizwa mahakamani.
Chadema kimesema uwepo wa wanachama na wafuasi wake mahakamani utakuwa ishara ya mshikamano na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo yenye maslahi kwa chama na wanachama wake.