White Frank, Mbunifu na mtafiti
UWEKEZAJI katika ubunifu na Teknolojia umeanza kuleta tija nchini. Ni baada ya White Frank, Mbunifu na mtafiti chakala cha kuku wa nyama kisichochanganywa na kemikali yoyote ambacho kitauzwa kwa bei rahisi na kitakuwa na tija. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Ubunifu huu umewezeshwa na serikali ya awamu ya sita kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).
White Frank, anasema kuwa kuwa chakula chake kitamwezesha mfugaji kupata kuku mwenye afya njema na mwenye kilo zinazohitajika sokoni.
Chakula hicho kinaleta matokeo ya haraka kwa wafugaji kwani ndani ya wiki tatu tu kuku amekuwa amefika kila moja na nusu na kilo mbili ikiwa tayari kwa ajili ya kufika sokoni.
White Frank analelewa na Costech tangu mwaka 2018 amefikisha wazo lake na Tume ikamwezesha kifedha na kiboresha wazo lake mpaka sasa linatarajia kuingia sokoni kama bidhaa.
Vyakula hivyo vinatengenezwa baada ya kufanyiwa utafiti wa kisayansi kwa mimea, wadudu, na nafaka.