RAIS wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitishwa kwa muda mfupi kwa operesheni ya kijeshi ya “Project Freedom” iliyokuwa inalinda meli na kusindikiza kupita katika Mlango wa Bahari wa Hormuz.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Trump alisema hatua hiyo imefikiwa kwa makubaliano ya pande zote kutokana na maendeleo mazuri katika mazungumzo kati ya Marekani na Iran.
Iran imepokea uamuzi huo kama ushindi, ikidai Marekani imelazimika kurudi nyuma baada ya kushindwa kufungua njia hiyo muhimu ya usafirishaji.
Trump pia alisema uamuzi wa kusimamisha operesheni hiyo umetokana na ombi la Pakistan, ambayo imekuwa ikisaidia upatanishi kati ya Marekani na Iran.
Hata hivyo, alieleza kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya bandari za Iran vitaendelea kubaki, huku hatua za baadaye kuhusu usalama wa usafirishaji katika Mlango wa Hormuz zikiwa bado hazijawekwa wazi.