RAIS wa Marekani Donald Trump amesema kuwa alikuwa na saa moja tu kabla ya kuidhinisha shambulio jipya dhidi ya Iran kisha kubadili uamuzi huo baada ya kupokea ombi kutoka kwa mataifa ya Ghuba kutofanya hivyo, huku akionya kuwa Marekani inaweza kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran siku chache zijazo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Trump amesisitiza kuwa viongozi wa Iran “wanatakiwa kuafiki makubaliano kwa haraka,” na kuongezea kuwa shambulio jipya la Marekani linaweza kufanyika siku chache zijazo iwapo hakutakuwa na makubaliano yaliyoafikiwa.
“Ninamaanisha ndani ya siku mbili au tatu, labda Ijumaa au Jumamosi au Jumapili, au mwanzoni mwa wiki ijayo, kwa sababu hatuwezi kuiruhusu Iran kuwa na silaha ya nyuklia.”
Trump pia alisema kuwa Rais wa China Xi Jinping aliahidi kutoipa jeshi la Iran silaha yoyote.
Jeshi la Iran nalo limejibu ujumbe huo wa Trump na kusema pia wako tayari kurejea kutekeleza mashambulizi.