SERIKALI ya Equatorial Guinea imejiuzulu baada ya makamu wa rais, Teodoro Nguema Obiang Mangue, ambaye pia ni mwana wa rais, kusema kuwa imeshindwa kutimiza majukumu yake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Nguema amesema kuwa Waziri Mkuu Manuel Osa, aliyeteuliwa mwaka 2024, tayari amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa baraza lake la mawaziri baada ya kutimiza asilimia 10 pekee ya malengo yaliyowekwa katika kipindi cha karibu miaka miwili.
Hata hivyo, chama tawala nchini humo, PDGE, kimesema kuwa kimefanikiwa kufikia malengo kadhaa, ila serikali ya sasa imelazimika kuondoka madarakani ili kutoa nafasi ya kuanza upya na kutekeleza malengo yanayohitajika kwa ufanisi zaidi.
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema, amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 na ni mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani, akifuatia Paul Biya wa Cameroon.