TAKA ozo zinazotokana na mabaki ya vyakula kama maganda ya matunda, mboga zilizooza, wali uliobaki na mabaki mengine ya jikoni zinaweza kuwa suluhisho kubwa la kulinda mazingira badala ya kuwa chanzo cha uchafuzi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mara nyingi taka hizi hutupwa hovyo na kusababisha harufu mbaya, kuziba mifereji pamoja na kuongeza uchafuzi wa mazingira. Hata hivyo, jamii inaweza kuzigeuza kuwa rasilimali yenye faida kubwa kiuchumi na kimazingira.
Njia mojawapo ya kutumia taka ozo ni kutengeneza mbolea ya asili (compost). Mabaki hayo hukusanywa na kuhifadhiwa sehemu maalumu ambapo huoza taratibu na kugeuka mbolea yenye virutubisho muhimu kwa mimea. Mbolea hii husaidia kuongeza rutuba ya udongo, kupunguza matumizi ya mbolea za kemikali na kuboresha uzalishaji wa mazao kwa njia rafiki kwa mazingira.
Aidha, taka ozo zinaweza kutumika kukuza nzi chuma, wanaojulikana kwa uwezo wao wa kula taka kwa haraka. Mabuu ya nzi hao hutumika kama chakula chenye protini kwa kuku na samaki, hivyo kusaidia kupunguza gharama za ufugaji. Baada ya mabuu kula taka, mabaki yanayobaki yanaweza kutumika tena kama mbolea ya asili mashambani.
Dk. Lucas Luchemba mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam tawi la Duce ndiye mtafiti aliyekuja na suluhisho la usafi wa mazingira na upatikanaji wa mbolea na chakula cha mifugo,Dk. Luchemba hakuishia hapo utafiti wake unajibu matakwa ya dira ya taifa ya 2025 kwa kuwa moja sekta yenye kutoa ajira nyingi,Dk. Luchemba anaweka wazi kuwa serikali imekuwa sehemu ya utafiti huo hasa kwa kulelewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech).
Huu utafiti WA Dr. Lukas Una faida za kiuchumi, kimazingira na kijamii. Anatakiwa kuwezeshwa au kutumiwa vyema na halmashauri na wizara ili afanye kwa mawanda mapana kufaidisha jamii.
Nimefurahi sana kuona Classmate wangu anavyo itumia taaluma kusafisha Mazingira kwa manufaa ya Taifa (afya, uchumi na elimu endelevu)