RAIS wa Kenya, William Ruto amesema wahalifu waliomshambulia Rachel Wandeto watachukuliwa hatua za kisheria bila kujali itikadi zao za kisiasa.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kupitia taarifa yake, Ruto amesema Kenya haina nafasi ya uvumilivu wa kisiasa unaozuia uhuru wa watu kutoa maoni yao au kushirikiana na wengine, akieleza kuwa vitendo vya namna hiyo vinatishia utulivu wa kidemokrasia wa nchi.
Kauli hiyo imekuja kufuatia tukio la kushambuliwa kwa Rachel Wandeto, ambaye Rais Ruto amemtaja kuwa mwanamke mwenye bidii na matumaini makubwa.