CHAMA cha ACT Wazalendo kimemteua Isihaka Mchinjita kuwa Waziri Mkuu wa Baraza Kivuli lililotangazwa leo 18 Mei 2026 na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Katika muundo huo mpya, Mchinjita anatarajiwa kuratibu mashambulizi ya kisera dhidi ya Serikali ndani na nje ya Bunge, akibeba sauti za chama hicho kwa wasemaji wa kisekta.
Mchinjita ni mwanasiasa mwenye ushawishi ndani ya chama hicho ambaye amekuwa mstari wa mbele katika uongozi na uratibu wa shughuli za chama, akipanda hadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bara.