KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza baraza kivuli la mawaziri huku akimteua Luhaga Mpina kuwa naibu waziri mkuu kivuli na waziri wa nishati na madini.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Semu ametangaza baraza hilo kivuli leo Jumatatu 18 Mei 2026 mbele ya waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mpina amewahi kuwa mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika utawala wa awamu ya tano, aliwahi kuwa waziri wa mifugo na uvuvi.
Mwaka 2025 katika mchakato wa urais ndani ya ACT-Wazalendo ilimchagua kuwa mgombea urais. Hata hivyo, hakuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika 29 Oktoba 2026.