Mafanikio ya kikundi cha vijana wanufaika wa mkopo wa asilimia nne wa Halmashauri kinachofahamika Mshikamano Group yamemvutia Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Ali Kawaida, kuwa mlezi wao na akiahidi kuendelea kufanya hivyo kwa vikundi vingine zaidi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kikundi hicho kinajishughulisha na ufyatuaji wa tofali kilipata mkopo Desemba 2025 wamefanikiwa kuongeza idadi ya ajira za vijana, kurejesha kwa wakati Sh 3.8 milioni, kununua mchanga wa kutoa huduma kwa kipindi kirefu .

Kawaida ameanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara ambapo atatembelea vikundi mbalimbali mkoani humo leo amezungumza na wana kikundi hao na kuwasihi kuendelea kurejesha mkopo wao wa Shilingi 50 milioni ili wengine wanufaike na kuwaahidi kuwaunga mkono.