Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji Puma Energy Tanzania (katikati)
KAMPUNI ya Puma Tanzania leo inatarajiwa kuzindua programu mpya ya ‘Puma PRIS’, ‘Aplikesheni’ ya kwanza nchini Tanzania ambayo imeletwa kwa lengo la kuwazawadia wateja kamilifu kwa huduma za mafuta na za rejareja, ikiwaweka wateja kitovu cha biashara yetu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari, Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji Puma Energy Tanzania alisema, uzinduzi huu unaunga mkono Mfumo wa Kimkakati wa Uchumi wa Dijitali Tanzania (2024–2034), unaolenga kuiweka nchi kama kitovu cha kidijitali cha kikanda kwa kuimarisha miundombinu, kupanua ujumuishaji wa kifedha, na kuendesha ukuaji wa uchumi.
Alisema Jukwaa hili linaruhusu wateja kupata zawadi kwa mafuta, vilainishi, na manunuzi kupitia maduka ya bidhaa mbalimbali yanayopatikana katika vituo vyetu, zinazoweza kutumika katika mtandao wetu wa rejareja – ikijumuisha mboga, vitafunwa, na huduma nyingine.

“PRIS ni mpango wetu wa kuwazawadia wateja duniani, tayari unawahudumia zaidi ya wateja milioni 2 katika Amerika ya Kusini. Kufuatia uzinduzi uliofaulu nchini Zimbabwe (Novemba 2025), Malawi (Februari 2026), na Botswana (Machi 2026), Tanzania inakuwa soko la nne barani Afrika kuzindua PRIS – programu-jumuishi ya zawadi kwa wateja,” Alisema Fatma.
Sulpis Mmasi, Meneja Mauzo ya Rejareja Puma Energy Tanzania alisema, mpango wa kuwazadia wateja utazinduliwa katika sehemu kubwa ya mtandao wetu wa awali, na utakamilika hivi karibuni.

“Mpango huu unakuza huduma salama na usiohitaji pesa taslimu kwa wateja kulingana na maono ya Tanzania ya uchumi wa kidijitali,” alisema Mmasi.
Lilian Kanora, Meneja Masoko Puma Energy Tanzania, alisema kwa kutumia zana za kidijitali, tunakuza ujumuishaji wa kifedha, kusaidia jamii za mitaa, na kuchangia ukuaji wa kijamii na kiuchumi.