Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza wasiwasi wake kuhusu hatua za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kikidai kuwa licha ya zuio dhidi ya chama hicho kuondolewa, bado kuna jitihada za kuzuia na kusimamisha shughuli zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza kufuatia mwenendo huo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema kuwa baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika 28 na 29 Aprili 2026 pamoja na matamko yaliyotolewa 2 na 5 Mei,2026, chama hicho kimepokea barua kutoka Ofisi ya Msajili ikikitaka kujieleza kuhusu masuala mbalimbali.
Mnyika amesema chama hicho kinaona hatua hizo kama mwendelezo wa jitihada za kuathiri utekelezaji wa shughuli za Chadema licha ya uamuzi wa awali wa kuondoa zuio hilo.
Aidha, Chadema imesisitiza kuwa itaendelea kufuata taratibu zote za kisheria na kusimamia haki na uhuru wa vyama vya siasa nchini.