KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu bado anaendelea na jitihada za kutaka kuunganishwa katika kesi inayohusu mgawanyo wa mali za chama hicho inayoendelea Mahakama Kuu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mnyika amesema awali Lissu aliwasilisha maombi mahakamani akiomba kuunganishwa katika kesi hiyo kama mtu binafsi, lakini maombi hayo yalitupiliwa mbali katika hatua za awali.
Mnyika amesema kwa sasa Lissu ameendelea na dhamira hiyo kwa kuwasilisha nia mpya ya kuunganishwa katika shauri hilo akiwa katika nafasi yake rasmi ya Mwenyekiti wa Chadema.
“Nataka kuwataarifu kwamba Mwenyekiti Tundu Lissu bado ameendelea na nia yake ya kuunganishwa kwenye kesi hii, awali alitaka kuunganishwa kama Tundu Lissu, sasa anataka kuunganishwa kama Mwenyekiti wa Chama,” amesema Mnyika.