WIZARA kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowezesha wanahabari wakongwe walioathiriwa na mfumo wa ithibati kurejea katika mfumo rasmi, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 ambayo ilitungwa kwa ajili ya kukuza taaluma ya uandishi wa habari kwa kuweka mfumo wa kitaasisi utakaosimamia sekta ya habari.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Mwongozo huu unaweka utaratibu wa kisheria wa kutambua na kuthibitisha umahiri wao kupitia tathmini maalumu ya uzoefu, weledi na maadili ya taaluma, na kuwawezesha kupata ithibati kwa mujibu wa sheria.
Spika, kupitia ushirikiano kati ya Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuwawezesha vijana wanaojiajiri katika sekta ya habari kwa kuwawezesha mitaji ya kukuza, kuendeleza na kuzalisha kazi zao katika ubora unaokidhi mahitaji ya soko kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
Katika kutekeleza hayo Rais Samia anatoa shilingi 20,000,000,000 kwa ajili ya Mfuko wa Utamaduni na tayari 2,000,000,000 kwa ajili ya mikopo kwa watengeneza maudhui mtandaoni (content creators) zimetoka kwa lengo la kuwasaidia kupata vitendea kazi na kuongeza uzalishaji wa kazi zao.
Amesema Paul Makonda wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo leo Bungeni Jijini Dodoma.