WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobass Katambi amemteua Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Godfrey Msongwe Kasekenya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza Hilo sambamba na Wajumbe 21.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 9, 2026 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, uteuzi huo umefanywa kwa mamlaka aliyonayo Waziri chini ya Kifungu cha 110 cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 (The Road Traffic Act, Cap 168) iliyorejewa mwaka 2023 ambapo uteuzi huo ulianza 15 Aprili 2026.
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani walioteuliwa ni pamoja na Prof. Hendry R. Sawe, Upendo James Mbele, Dk. Baghayo A. Saqware, Dk. Phil M. Kierru, Augustus Emmanuel Fungo, Mhandisi Mohamed Besta, Mhandisi Yona Afrika Mwampagatwa, Mhandisi Victor H. Seff na Issa Kassim Nkya.
Wengine ni Abdul M.Maulid., Ramadhan Seleman, Isabella Oswald Nchimbi, Faraj Jaffa Abri Asas , Jackson Nghoboko Bulashi, Salma Ali Bakar, Malk Hamad Bakari, Said Kassim Kagomba, Robert Mwinje, na Mhandisi Kashinde Shabani Mussa.