JESHI la Polisi mkoani Katavi linawashikilia askari saba wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mwalimu wa Shule ya Msingi Kamsisi, Une Mwakabange (42), aliyepigwa risasi 6 Mei 2026 ndani ya Pori la Inyonga wilayani Mlele.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, askari hao walikuwa katika doria walipowaona watu watatu wakiwa na pikipiki na kujaribu kuwafukuza. Katika tukio hilo, askari James Daniel (25) anadaiwa kufyatua risasi iliyompiga Une mguuni na kuanguka chini.
Imeelezwa kuwa baada ya kujeruhiwa, Une alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia akiwa njiani.Jeshi la Polisi limeendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku askari hao wakishikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.