SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa virusi vya Hanta si mwanzo wa janga la kimataifa, huku likisisitiza kuwa linaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali kuhakikisha abiria waliokuwa katika maeneo yaliyoathirika wanarejea kwao salama baada ya kufanyiwa vipimo vya kimatibabu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea
Mkuu wa WHO amesema kiwango cha hatari katika Visiwa vya Canary nchini Hispania bado ni cha chini, akiongeza kuwa hatua za tahadhari na ufuatiliaji zinaendelea kuchukuliwa ili kudhibiti maambukizi hayo yasienee zaidi.Aidha, alimshukuru Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sánchez, kwa msaada na ushirikiano unaotolewa katika kukabiliana na hali hiyo.
Wakati huo huo, bara la Afrika limeathiriwa moja kwa moja na mlipuko huo ambapo baadhi ya wagonjwa wameendelea kupatiwa matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini
Akizungumza na waandishi wa habari nchini Ghana, Profesa Mohammed Janabi alisema hali hiyo inahitaji mwitikio wa kimataifa unaoratibiwa kwa pamoja pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya afya ili kuzuia madhara makubwa zaidi.