MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) imetangaza bei za mafuta kwa mwezi Mei 2026 zitakazoanza kutumika kuanzia leo Alhamisi 7 Mei 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Katika taarifa iliyotolewa jana 6 Mei 2026 usiku na Zura, bei ya mafuta ya dizeli na petroli imeongezeka ambapo lita moja ya petroli imepanda kutoka Sh3,500 za Aprili hadi Sh3, 820 sawa na ongezeko la Sh320.
Lita moja ya dizeli itauzwa Sh3, 850 kama ilivyo petroli ikilinganishwa na Sh3, 500 sawa na ongezeko la Sh350 huku mafuta ya taa yakiuzwa Sh3, 850 sawa na ongezeko la Sh350.
Taarifa hiyo imeleza sababu ya kupamba kwa bei hizo ni kuongezeka kwa bei ya ununuzi wa mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji kutoka katika soko hilo hadi kufika Zanzibar.
Mkazi wa Darajani, Mohammed Salah amesema Serikali inapaswa kuweka mpango madhubuti wa kuhifadhi mafuta na si kutegemea kununua nje kila siku.
Naye Salma Hamid amesema Serikali inatakiwa kupunguza bei ya kodi kwa mafuta, kwani awali walisema mafuta yapo ya kutosha na kuwatoa hofu wananchi lakini anashangazwa kuona ongezeko hilo kwa wakati huu.