RAIS wa zamani wa Andry Rajoelina huenda akafikishwa mahakamani hivi karibuni kufuatia dhamira ya Serikali mpya ya Madagascar kuchukua hatua za kisheria dhidi yake.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Waziri wa Sheria wa nchi hiyo alitoa kauli hiyo Jumanne 5 Mei wakati wa ufunguzi wa kikao cha kawaida cha Bunge, akisisitiza kuwa mamlaka mpya zimedhamiria kuhakikisha kuwa mchakato wa sheria unatekelezwa dhidi ya kiongozi huyo wa zamani.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, licha ya kutotolewa kwa maelezo ya kina kuhusu mashtaka yanayoweza kumkabili, Serikali imeanza kuongeza shinikizo ili kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Rajoelina aliondolewa madarakani mwezi Oktoba 2025 na kwa sasa anaishi uhamishoni katika mji wa Dubai.