MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche, amesema elimu ni muhimu, lakini haina manufaa makubwa ikiwa haiwezi kutumika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ya Chadema (CHASO) mkoani Iringa, Heche alisema chama hicho kikiingia madarakani kitaboresha mfumo wa elimu ili kujenga vijana wenye uwezo wa kuhoji, kudadisi, kufuatilia na kusimamia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya jamii na taifa.
Alisema lengo ni kuwa na mfumo wa elimu unaozalisha wahitimu wenye fikra huru, ubunifu na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.