MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche, amesema vijana wengi wanakaribia chama tawala kwa sababu wanaamini kuwa mwanachama wa CCM kunawapa fursa zaidi za ajira, huku wakihofia kuwa kujiunga na upinzani kunaweza kuwanyima nafasi hizo au kuwaweka katika hatari.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Heche amesema vijana ndiyo taifa la kesho na wanahitaji mabadiliko yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika kujenga mustakabali wao na wa nchi.Heche ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vijana wa CHASO mkoani Iringa