MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, leo 2 Juni 2026 amewasili Kilwa Kivinje mkoani Lindi kwa ajili ya kushiriki shughuli mbalimbali za chama kabla ya mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika kesho, 3 Juni 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mara baada ya kuwasili, Heche aliongoza zoezi la kupandisha bendera za chama katika vizimba mbalimbali vya Chadema vilivyopo Kilwa Kivinje, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha shughuli za kisiasa na kuongeza hamasa kwa wanachama na wananchi wa eneo hilo.
Kesho, Heche anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Kilwa Kivinje, ambapo viongozi wa chama wanatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo ya taifa.