MSEMAJI wa Jeshi la Magereza nchini, Elizabeth Mbezi, amesema anafuatilia kupata majibu sahihi juu ya taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema)Tundu Lissu atagoma kula kuanzia keshokutwa (tarehe 26 Oktoba 2026).Anaripoti mwandishi wetu, Dar es salaam … (endelea)
Kwa mujibu wa mawakili wa Lissu mteja wao ameamua kuchukua hatua hiyo ili kushinikiza uongozi wa gereza la Ukonga kumtendea haki kwa kumpa nafasi azungumze na mawakili wake bila kuwapo askari.
Akizungumza na Mwanahalisi Digital leo 24 Oktoba 2026, Mbezi amejibu kwa ufupi kuwa taarifa hizo bado hana hivyo anazifuatilia.
“Taarifa hiyo mimi sina ngoja niifuatilie kwa sababu nipo Dodoma na yeye yupo Dar es Salaam”amesema Mbezi
Taarifa za mgomo wa kula wa Lissu zimetolewa leo 24 Oktoba 2026 na Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Dk.Rugemeleza Nshala wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mwisho.