HATIMAYE uongozi wa Yanga sports club, umetangaza kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa Manqoba Mngqithi,Leo tarehe 22, Oktoba, 2026.Anaripoti mwandishi wetu, Fedrick Gama Dar es salam … (endelea)
Klabu hiyo pia imeachana na aliyekuwa kocha wa viungo wa timu hiyo ya kwanza Chyna Mokaila
Uamuzi huo umefanyika kutokana na mwenendo usiokuwa mzuri wa klabu hiyo katika michezo kadhaa iliyocheza hivi karibuni.
Yanga katika mechi ambazo imecheza hivi karibuni ni pamoja ile ya mtani wake wa Kariakoo, Simba Sc ambapo ilifungwa magoli 2-1, mechi ya ya TRA United waliyotoka sare ya 0-0

Matokeo haya ndio sababu ya klabu hiyo kufanya uamuzi huo Kwa makocha Mangqoba Mngqithi kufika mwisho.
Kuondolewa kwa kocha huyo kulitarajiwa na baadhi ya mashabiki waliokuwa wakiushinikiza uongozi umfute kazi kocha huyo.
Mashabiki hao walikuwa wakilaumu kikosi chao kinavyocheza na mabadiliko yaliyokuwa yakifanyika.
Mwisho.