SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), kwa kushirikiana na wananchi, limehakiki mipaka kati ya hifadhi ya taifa Nyerere na maeneo ya wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.Anaripoti mwandishi wetu, Arusha… (endelea).
Uhakiki huoi ni utekelezaji wa tangazo la Serikali No. 595 la Tarehe 3/10/2025 (Government Notice – GN), hatua inayolenga kuweka uelewa wa pamoja kuhusu mipaka ya hifadhi na maeneo yanayozunguka hifadhi hiyo.
Katika zoezi hilo, maofisa wa TANAPA wakiongozwa na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Ephraim Mwangomo, wamehusika katika uhakiki wa mipaka pamoja na wananchi katika maeneo husika.

Uhakiki huo limewashirikisha viongozi wa halmashauri, madiwani, wenyeviti wa vijiji na mitaa, kwa lengo la kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa ushirikiano na uelewa wa pande zote.
Uhakiki huo unaweka msingi wa kuwa na mipaka inayofahamika kwa wananchi na mamlaka za uhifadhi, hatua inayoweza kusaidia kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi na kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi.
Mwisho.