MFANYABIASHARA maarufu nchini Zimbabwe na swahiba wa viongozi kadhaa wa Afrika, Wicknell Chivayo, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Chivayo amekutwa na mauti kufuatia ajali mbaya ya helikopta huko Marondera, mashariki mwa jiji la Harare nchini Zimbabwe.
Serikali ya Zimbabwe kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Nick Mangwana, imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha helikopta iliyokuwa imebeba abiria sita ikijumuisha marubani wawili, wafanyabiashara, na abiria wengine.
Mamlaka zote ikiwemo Jeshi la Polisi la Zimbabwe (ZRP) zimebainisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyenusurika kwenye ajali hiyo iliyotokea majira ya saa kumi na moja jioni kwa saa za Zimbabwe.

Taarifa za karibu zinasema kuwa mke wa Chivayo, Lucy Muteke, pia ni miongoni mwa watu sita waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Wicknell Chivayo, anayejulikana pia kama Sir Wicknell, amekuwa mtu mashuhuri nchini Zimbabwe na kanda ya Afrika Mashariki na Kusini kutokana na biashara zake, ukwasi mkubwa.