MAHAKAMA Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam iko ukingoni kuamua hatma ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo imebaki nafasi moja ya pande zote ile ya mashtaka na ya utetezi kuwasilisha hoja zao za mwisho.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hoja za Lissu ni za kujitetea kuieleza mahakama hiyo kuwa hataki kuendelea kushikiliwa wala kuhukimiwa badala yake anataka kurejea nyumbani kwake kwa kutoa rejea za kesi mbalimbali za kesi na hukumu zake sambamba na sheria.
Hivyo kwa upande wa Serikali kueleza kwanini Lissu aadhibiwe nao ukieleza jinsi ya ulivyokusanya ushahidi na kurejea kesi mbalimbali.
Wakili Edson Kilatu akizungumza na MwanaHALISI ameeleza kuwa hatua hiyo inatoa nafasi kwa mshtaki kugongelea msumari wa mwisho juu ya ushahidi na hoja zake lakini pia kwa mshtakiwa kueleza kuwa ushahidi uliowasilishwa na Jamhuri sio chochote.
Wakati huo huo ameeleza nafasi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuamua kuachana na shauri hilo kwamba wakati wowote kabla ya hukumu kusomwa.