TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshtakiwa kwa tuhuma uhaini kwenye Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, anatajwa kuwa ni miongoni mwa wanasiasa mwenye kutazamwa kwa jicho la kipekee na dunia.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yameelezwa na Mchambuzi wa masuala ya siasia nchini, Saliely Sallema amesema kuwa Lissu ni mmoja wa wanasiasa wenye heshima duniani ndio amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vyama vya Demokrasia duniani ambapo hatma yake kwenye shauri hilo inaweza kuiathiri Tanzania kwenye mawanda ya kidunia.
Sallema, amesema kuwa Lissu ni mwiba mkali kwa serikali ndio maana amejikuta kwenye mikono ya dola ili kudhibitiwa lakini hakuna jambo baya litakalomkuta kwa kuwa masikio ya macho ya dunia yanasubiri hatma yake ili nao wafanya uamuzi juu ya suala hilo.