MWENYEKITI wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Jaji Shaban Ally Lila, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Tume hiyo inaenda kutekeleza kazi iliyoelekezwa ya kuchunguza na kubaini wahusika wa ghasia za Uchaguzi Mkuu wa 2025.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Tume hiyo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuchunguza matukio ya ghasia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kufuatia mapendekezo ya Tume ya Rais iliyochunguza matukio ya uvunjifu wa amani.
Jaji Lila anaongoza Tume hiyo akisaidiwa na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.
Mkutano huo na waandishi wa habari unatarajiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kazi ya Tume, hatua iliyofikiwa na masuala yanayohusiana na uchunguzi wake