JAJI wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Kijinai kuhusu matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025, Jaji Shabani Ally Lila, amewataka wananchi wenye taarifa au ushahidi kuhusu machafuko hayo kuwasilisha mbele ya Tume.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Jaji Lila ameeleza kuwa Tume itatumia njia mbalimbali katika kukusanya taarifa na ushahidi kutoka kwa wananchi ili kusaidia uchunguzi wake kuhusu matukio hayo.
Amesema wananchi wenye taarifa muhimu wanaweza kuwasilisha ushahidi wao kupitia barua pepe Barua@tumeuchaguzi.go.
Aidha, Jaji Lila amesema Tume iko tayari kuweka utaratibu wa kuhakikisha wananchi wenye ushahidi wanafika mbele ya Tume kutoa maelezo, bila kujali walipo.
Jaji Lila ametoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa au ushahidi unaoweza kusaidia katika uchunguzi huo kuwasilisha taarifa hizo kwa Tume ili ziweze kufanyiwa kazi katika mchakato wa uchunguzi.