SERIKALI imesaini mkataba wa uwekezaji wa madini ya Kinywe wenye thamani ya Sh. 265 Bilioni huku iikikabidhiwa umiliki wa hisa za asilimia 17. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).
Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema hayo leo kabla ya kusaini mkataba wa madini ya kinywe dhidi ya Kampuni ya Mgodi ya kichina (YUDI) wenye thamani ya shilingi Bilioni 265 katika eneo la mgodi uliopo kwenye kijiji cha Mbwade Kata na Tarafa Bwakira Chini wilayani Morogoro.
Waziri Mavunde amesema madini hayo yenye uwezo wa kutengeza vifaa mbalimbali vya umeme ikiwemo betri za umeme za magari yanapatikana maeneo mengi duniani ikiwemo nchi za China, Madagascar na Tanzania.
Waziri huyo amesema nchi ya China inaongoza kwa kuzalisha tani Milioni 1.4 duniani na kwa Bara la Afrika nchi ya Madascar inayozalisha tani 90,000 inaongoza ikifuatiwa na Tanzania inayozalisha tani 75,000 zinazotoka kwenye miradi miwili pekee.
Amesema miradi yote ikikamilika Tanzania itawshika nafasi ya kwanza kuwa mzalishaji mkubwa wa madini.
Mavunde amesisitiza wawekezaji hao kuonesha thamani kwa jamii kwa kutekeleza wanayopaswa kisheria ikiwemo kutoa ajira kwa watanzania hasa wanaoishi maeneo ya mradi wakiwemo wakimama na vijana.
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Zuberi Mfaume amewaomba wawekezaji hao kuona haja ya kusimamia shughuli za uwekezaji mkubwa wa mradi madini sambamba na kuwa na mradi mkuwa wa maji sababu maji yaliyopo hayakidhi hata mahitaji ya wananchi wa Kata hiyo.
Pia Mfaume amewaagiza wawekezaji hao kuzingatia masuala ya uhifadhi wa mazingira wakati wakitekekeza mradi huo ili kuepuka kuharibu vyanzo vya maji vilivyopo na pengine kuvifukia na vifusi na kuteteresha bwawa la maji Kidunda ambalo limejengwa kwa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya manufaa ya wananchi.
Balozi wa China Liu Xiaoming amesema mradi huo mkubwa ulioleta mahusiano zaidi baina ya China na Tanzania utasaidia kutoa ajira zaidi kwa watu zaidi ya 500 kwa watanzania huku ukileta maendeleo kwa mmoja mmoja na nchi nzima kwa ujumla.
Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini mkoa wa Morogoro Dk Mzeru Nibuka ameiomba serikali kupanga bei ya madini ya wachimbaji wadogo ili kuondoa kero na kudhurumika wanapofikisha kwenye kampuni za wawekezaji.
Pia ameiomba serikali kuongeza juhudi ya kufanya tafiti kwenye milima hiyo na kuendelea kubaini uwepo wa madini mengi zaidi katika maeneo ya milima kama ilivyokuwa kwa miradi hiyo ili wananchi wa Morogoro na Tanzania nzima kwa ujumla wanufaike.