MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania leo tarehe 30 Julai 2026 imetoa uamuzi kwenye kesi ya mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Tundu Lissu ( criminal Revision no. 7203216/2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(end
Katika maombi hayo Jamhuri waliomba mahakama ya Rufaa kufanya marejeo dhidi ya taarifa ya kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba kwenye kesi ya Uhaini inayomkabili Mhe Lissu.
Mtakumbuka kwamba, Lissu aliweka pingamizi na mahakama kuu ikakubaliana naye kwa kukataa ushahidi mpya kuingizwa mahakamani, kitendo kilichopelekea Jamhuri kusajili nia ya kukata rufaa lakini baadaye wakasajili maombi ya marejeo.
Tarehe 3 Julai 2026 Mahakama ya Rufaa ilisikiliza maombi hao na leo kwa njia ya mtandao Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali maombi ya DPP ikisema mahakama kuu walikuwa sahihi kuitupilia mbali taarifa ya kusudio la kuongeza ushahidi mwingine chini ya kifungu cha 308 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai.
Mahakama ya Rufaa pia imekataa hoja ya DPP kwamba hakusikilizwa na imeyatupilia mbali maombi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini.
Kwa sababu hizo, kesi ya uhaini dhidi ya Lissu inapaswa sasa kuendelea mahakama kuu.
