MWENYEKITI wa Chadema, Tundu Lissu, na Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, leo 22 Julai 2026 wamekutana kwa mara ya kwanza tangu mwanasiasa huyo arejee ndani ya chama hicho akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM).Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Wawili hao walionekana wakikumbatiana katika viwanja vya Mahakama Kuu, Dar es Salaam, mara baada ya kesi iliyofunguliwa na mawakili wawili wanaojitambulisha kuwa washauri wa kisheria wa Lissu kuahirishwa kwa muda.
Msigwa alifika mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, ambayo inahusu pingamizi dhidi ya kile mawakili hao wanachodai ni kuzuiwa kwa haki yao ya kufanya mashauriano ya siri na mteja wao akiwa Gereza la Ukonga.
Mkutano huo umevutia hisia za wanachama na wafuasi wa Chadema, ukizingatiwa kuwa ni wa kwanza kati ya viongozi hao tangu Msigwa atangaze kurejea rasmi ndani ya chama hicho 23 Mei 2026.
Msigwa, ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, alihamia CCM mwezi Juni 2024 kabla ya kurejea tena Chadema baada ya takribani mwaka mmoja.
Kesi hiyo imeahirishwa kwa muda, huku ikitarajiwa kuendelea kusikilizwa katika tarehe itakayopangwa na mahakama.