JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kumkamata Mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya Watu wawili waliokuwa wamefukiwa ndani ya eneo la nyumba yao Mtaa wa Sindano, Mwananyamala Jijini Dar es salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, Mtuhumiwa, Hosamu Hamza maarufu Maopena amekamatwa 17 Julai 2026 majira ya saa 9 alasiri eneo la Makongo akiwa na kisu kilichokuwa na damu pamoja na mavazi yaliyokuwa yamechafuka damu na kupelekwa kituo cha Polisi kwa mahojiano.
Baadaye usiku, Polisi walipokea taarifa kutoka kwa Wananchi kuwa Watu watatu waliokuwa wanaishi nyumba moja Mtaa wa Sindano walikuwa hawaonekani, huku kukiwa na damu nyingi ndani ya nyumba hiyo.
Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika ulibaini kuwa Watu wawili, Hamza Juma Omari (Mautila), mwenye umri wa miaka 48, na Ally Juma Omari, mwenye umri wa miaka 37, walikuwa wameuawa na kufukiwa ndani ya shimo katika eneo la nyumba hiyo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mtuhumiwa Hosamu Hamza Juma (Maopena), ambaye ni Mtoto wa marehemu Hamza Juma Omari, ndiye anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ya Baba yake mzazi pamoja na Baba yake mdogo kabla ya kuwafukia ambapo Polisi wamesema sababu za tukio hilo bado zinaendelea kuchunguzwa.