KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amewataka wananchi kuwa na matumaini nao, kwani hatua tuloifikia ni kubwa na mwanzo mzuri wa safari ya kumaliza kabisa tatizo la Zanzibar linalotokana na uwaniaji madaraka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Kule ndani tulipokuwa tukizungumza hakukuwa na mizinga lakini hekaheka zilikuwa tele. La muhimu baada ya majadialiano tulikubaliana na tukasonga mbele.
Msisitizo wetu wakati wote ilikuwa kutanabahisha kuwa kwani Zanzibar hatuna tatizo? Hivi kumvisha mtoto wa skuli sare za jeshi akapewa makaratasi na kupelekwa kwenda kupiga kura, si tatizo hili? Huyu mtoto utamkataza vipi akiwa skuli kuiba au kufanya udanganyifu wakati wa mtihani? Tukakubaliana tatizo tunalo.
Basi tujadiliane tukijua fika lazima kuzingatia maslahi ya Zazibar na watu wake. Mimi na Babu Othman hatukubali kuona jamii yetu inavurugwa. Tumepita kwingi watu wakiuliwa. Ilianza vita vya ng’ombe, vikaja vya Juni na yakaja mauaji hivi 2001.
Hapa 2020 wakauliwa watu 21. Mpaka lini watu waendelee kuuliwa kwa sababu ya watu wachache kung’ang’ania madaraka? Safari hii tunatumainia haitakuwa “yaleyale” kwa sababu tunayo ratiba ya utekelezaji mambo tuliyokubaliana.
Idara ya Oganaizesheni andaeni haya makubaliano katika njia rahisi na kuyapeleka kwa wananchi wayajue.