MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama Rufani leo tarehe 3 Julai 2026 ambapo anatarajiwa kuchuana na jopo la mawakili wa Serikali kwa hoja za kisheria wakati wa usikilizwaji wa shauri lililofunguliwa dhidi yake na Jamhuri, kuhusiana na kesi ya uhaini inayomkabili.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Jamhuri ilifungua shauri hilo la maombi ya mapitio 24 Februari 2026, ikipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, kuikatalia maombi yake ya kutaka iruhusiwe kuwasilisha ushahidi wa nyongeza katika kesi ya uhaini inayomkabili mwanasiasa huyo.
Shauri hilo la mapitio namba 7203216/2026 limepangwa kusikilizwa leo, Ijumaa 3 Julai 2026, na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani litakaloketi Dar es Salaam, linaloongozwa na Jaji Augustine Mwarija, Majaji wengine ni Zainabu Muruke na Amour Khamis.